Wakulima wawa na pilika nyingi za shambani katika sehemu ya mji mdogo Yuchi, Chongqing (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 08, 2026
Wakulima wawa na pilika nyingi za shambani katika sehemu ya mji mdogo Yuchi, Chongqing
Mkulima akipandikiza miche ya mpunga kwenye shamba la mpunga katika sehemu ya mji mdogo Yuchi wa Wilaya inayojiendeshaya Kabila la Watujia ya Shizhu, huko Chongqing, kusini magharibi mwa China Mei 7, 2026. (Xinhua/Tang Yi)

Mji Yuchi huko Chongqing, kusini magharibi mwa China ni mji mdogo wa shughuli haswa za kilimo, mji huo mdogo uko kwenye eneo lenye wastani wa mwinuko wa mita 1,000 kutoka usawa wa bahari, ambapo mashamba yake ya kilimo yaliyojengwa kwa kufuata kigezo cha juu yamefikia hekta 866.67 katika miaka ya hivi karibuni, na kuwa kundi la kwanza la mashamba ya kielelezo ya kiwango cha juu katika maeneo ya vilima ya mji huo mdogo. Mavuno ya mwaka ya mpunga wenye ubora wa juu ya mashambani yanazidi tani 3,700.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha