Lugha Nyingine
Mji wa Shenzhen waongoza maendeleo ya uchumi wa anga ya chini wa China (4)
Mji wa Shenzhen ambao ni kituo cha teknolojia, Kusini mwa China hivi sasa umekuwa kituo kinachoongoza uundaji wa vyombo vya urukaji kwenye anga ya chini vinavyojiendesha vyenyewe, ukizalisha asilimia 70 ya droni za matumizi ya watu na asilimia 50 ya droni za matumizi viwandani nchini China.
Upanuzi wa sekta ya uchumi wa anga ya chini ya Shenzhen unachochewa na uwekezaji unaozidi kuongezeka wa mji huo katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia. Kuanzia mwaka 2020 hadi 2024, uwekezaji wa jumla wa Utafiti na Maendeleo (R&D) wa Shenzhen uliongezeka kutoka yuan bilioni 151.08 hadi yuan bilioni 245.31, na wastani wa ongezeko la mwaka umefikia asilimia 12.9.
Uchumi wa anga ya chini wa China umepata maendeleo ya kasi kubwa tangu kutambuliwa kwake kuwa kichocheo kipya cha ukuaji katika ripoti ya kazi ya serikali ya 2024.
Mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030) wa China umesema kuwa, ni lazima kuhimiza maendeleo mazuri na yenye utaratibu ya uchumi wa anga ya chini, kuboreshwa kwa usahihi usimamizi wa nafasi kwenye anga ya chini, na kufanya juhudi za kupanua matumizi ya anga ya chini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




