Lugha Nyingine
Mkutano wa Intaneti Duniani wa Asia-Pasifiki wafunguliwa Hong Kong ili kukusanya maoni ya pamoja kuhusu mkakati wa kidijitali
HONG KONG - Mkutano wa siku mbili wa Intaneti Duniani 2026 wa Asia na Pasifiki umefunguliwa rasmi jana Jumatatu katika Hong Kong, China, ukiwakutanisha watunga sera, viongozi wa sekta ya kidijitali na wasomi kutoka nchi na maeneo 50 duniani kwa ajili ya kujadili mkakati wa pamoja wa kidijitali katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwenye nafasi za mtandao.
"Kuandaa mkutano huu kumeonesha wazi nafasi inayozidi kuongezeka ya Hong Kong ikiwa kituo cha kimataifa cha uvumbuzi na teknolojia," John Lee, ofisa mtendaji mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong, amesema wakati akihutubia tukio hilo.
"Tunaweka pamoja mkakati wa jumla wa kuunganisha miundombinu ya kiwango cha juu cha dunia, utafiti na maendeleo ya teknolojia mpya za hali ya juu na utamaduni wa uvumbuzi wenye kuwajibika," Lee amesema, akielezea juhudi za kuboresha nguvu ya mambo ya kompyuta ya Hong Kong na kuifanya teknolojia ya AI kuleta manufaa kwa wote.
Mkutano huo wa mwaka huu utajadili mafungamano ya teknolojia za kidijitali na mambo ya fedha, afya na uhifadhi wa mali za urithi wa kitamaduni, na pia kutoa majukwaa kwa ajili ya mijadala kati ya sekta za umma na za kibinafsi.
Ren Xiangliang, katibu mkuu wa Mkutano wa Intaneti Duniani, amesema kwenye mkutano huo kwamba, Hong Kong ikiwa ni "kiunganishi bora zaidi" na "kiongeza thamani kikubwa zaidi," inajenga na kukuza mifumo iliyoratibiwa, yenye ufanisi mkubwa na kufanya kazi kwa kufuata hali halisi ili kutoa uwezo, raslimali na haki kwa kampuni za sayansi na teknolojia.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
