Lugha Nyingine
Habari picha: Mjumbe wa Bunge la Umma la China aufanya ufundi wa udarizi wa kikale wa kabila la Wayi kuwa wa kisasa
Jin Ruirui, mkuu wa shirikisho la mafundi wa kudarizi la kabila la Wayi la ngazi ya kiwilaya katika Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, amekuwa akijikita katika kuhifadhi ufundi huo wenye historia ya miaka zaidi ya elfu moja, wakati huohuo amewaongoza mafundi wenyeji wa kudarizi kuelekea ustawi wa kitamaduni na ustawishaji wa vijiji.
Ufundi huo wa kudarizi wa kabila la Wayi wenye historia ya miaka ya zaidi 1,300, unajulikana kwa udarizi wake wa michoro na picha za kupendeza na mbinu mbalimbali za kudarizi, na umekuwa kibebaji muhimu cha utamaduni wa kabila la Wayi.
Katika miaka mingi iliyopita, Jin amesaidia wanawake zaidi ya 2,000 kupata kazi. Kupitia juhudi zao, ufundi huo wa kikale umetoka milimani na kuonekana kwenye majukwaa ya wiki za mitindo katika miji ya Milan, New York na Paris. Kwa kupitia mafungamano kati yake na usanifu wa kisasa wa mitindo, ufundi huo umepanuka siku hadi siku kwenye masoko mapya na kufikia hadhira mpya.
Mwaka 2023, Jin alichaguliwa kuwa mjumbe wa Bunge la Umma la China (NPC). Akiwa mjumbe, ametoa mapendekezo juu ya masuala kama vile ulinzi wa ufundi huo wa kudarizi wa kabila la Wayi na maendeleo husika ya viwanda, ajira, elimu, na matibabu.
Kwenye "mikutano mikuu miwili" ya China ya mwaka huu, Jin atafuatilia zaidi ukuaji wa viwanda vya ufundi wa kudarizi wa kabila la Wayi, afya ya kisaiklojia ya vijana na kuzuia uhalifu wa vijana wa chini ya umri wa miaka 18.

"Tamasha la Maolong" la kabila la Wayilao lasherehekewa kwa ngoma ya dragoni mkoani Guizhou, China

Mji mkongwe wa Wuzhen, China wazindua shughuli mbalimbali wakati wa Mwaka Mpya wa Jadi wa China

Hong Kong Yasherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Farasi wa China kwa Maonyesho ya Fataki

Ufunguzi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan-Cortina mwaka 2026
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
