Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China wafunguliwa Beijing

(CRI Online) Machi 04, 2026
Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China wafunguliwa Beijing
(Picha/Xinhua)

Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China umefunguliwa rasmi leo Machi 4 saa tisa mchana katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing. Katika mkutano wa siku saba, wajumbe 2,078 kutoka nyanja 34 ikiwemo uchumi, utamaduni, elimu na raslimali za mazingira watasikiliza na kupitia ripoti ya kazi ya baraza hilo na ripoti kuhusu kazi ya utoaji mapendekezo, huku wakihudhuria mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la Taifa, kusikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya serikali na ripoti nyingine husika, kujadili mswada wa mwongozo wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii.

Mfumo wa ushirikiano kati ya vyama vingi na mashauriano ya kisiasa unaoongozwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ni mfumo wa kimsingi wa siasa wa China. Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China ni chombo muhimu ambacho wajumbe kutoka vyama tofauti vya kisiasa, asasi mbalimbali za kiraia, makabila madogomadogo na nyanja mbalimbali za jamii hufanya mazungumzo ya kidemokrasia kuhusu mipango mikakati ya taifa chini ya uongozi wa CPC. Kupitia mfumo huo, vyama mbalimbali vya kisiasa, asasi mbalimbali za kiraia, wajumbe kutoka nyanja mbalimbali za jamii wanashiriki kwenye mazungumzo na mijadala kuhusu mambo ya taifa, kutimiza ushiriki jumuishi wa pande mbalimbali katika mambo ya siasa na mashauriano ya kidemokrasia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha