Mjumbe wa Bunge la Umma la China awasilisha sauti za viwandani za mashinani (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 03, 2026
Mjumbe wa Bunge la Umma la China awasilisha sauti za viwandani za mashinani
Guo Hongjing akikagua vitu na raslimali kwenye kiwanda cha Kampuni ya Matairi ya Tianjin Lizhong mjini Tianjin, kaskazini mwa China, Februari 25, 2026. (Xinhua/Li Ran)

Guo Hongjing anafanya kazi ya mkuu wa timu ya vipuri vya vifaa katika idara ya ghala ya Kampuni ya Matairi ya Tianjin Lizhong mjini Tianjin, kaskazini mwa China. Kazi yake ya kila siku ni kupokea, kutoa na kukagua raslimali ndani ya ghala. Kazi hiyo inayoonekana kuwa ndogo si rahisi hata kidogo. Kuanzia skrubu hadi mota, katika aina na modeli zote, lazima atunze na kukumbuka kila kitu ndani ya ghala.

Tangu mwaka 2018, Guo amechaguliwa kwa awamu mbili mfululizo kuwa mjumbe wa Bunge la Umma la China (NPC), akiwa mjumbe wa Bunge la Umma, amekuwa akiwajali zaidi wafanyakazi wenzake. Anasikiliza sauti za wafanyakazi wa mstari wa mbele na kukusanya maoni na mapendekezo yao kadiri awezavyo.

Wakati wa kuwa mjumbe huo, Guo ametembelea kampuni za viwanda kufanya utafiti na kujionea hali halisi, huku akifuatilia zaidi uboreshaji wa viwanda na mabadiliko ya hali ya kazi za wafanyakazi wa viwandani. Pia ametoa mapendekezo kuhusu utunzaji wa wazee wa vijijini na masuala ya faragha yanayohusiana na uvujaji wa taarifa za bili za wateja kupitia vifurushi vya mizigo vinavyosafirishwa na kampuni husika. Kwenye "mikutano mikuu miwili" ya China ya mwaka huu, Guo ataweka msisitizo juu ya maendeleo ya kijani ya viwanda, ulinzi wa haki na maslahi ya wafanyakazi, na utekelezaji wa sera ya likizo bila kupunguza mshahara. 

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha