Chapa ya simu za mkononi ya Honor ya China yazindua Simu Roboti kabla ya MWC 2026 (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 02, 2026
Chapa ya simu za mkononi ya Honor ya China yazindua Simu Roboti kabla ya MWC 2026
Watu wakitazama "Simu Robot" kwenye tukio la uzinduzi wa bidhaa duniani mjini Barcelona, Hispania, Machi 1, 2026. (Xinhua/Cheng Min)

BARCELONA, Hispania - Chapa ya teknolojia ya Honor ya China jana Jumapili imezindua kile ilichokiita "Simu Roboti" ya kwanza katika sekta ya mawasiliano ya simu kabla ya Mkutano wa Simu za Mkononi wa Dunia 2026 mjini Barcelona, Hispania na kutambulisha dhana yake mpya ya Akili ya Binadamu Iliyoongezwa Uwezo (AHI).

Kwenye hafla ya uzinduzi wa bidhaa duniani, Afisa Mtendaji Mkuu wa Honor Li Jian amesema Simu hiyo Roboti ina mfumo wa kamera ya gimbal ya mihimili mitatu wa kwanza katika sekta hiyo uliojumuishwa kwenye simu janja, akiuelezea kuwa ni aina mpya ya simu janja.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, bidhaa hiyo inaunganisha uwezo mkuu wa aina mbili wa AI - maingiliano na AI kwenye roboti na upigaji picha wa kiwango cha juu – ili kuwapa watumiaji kile kampuni hiyo ya Honor inachokiita matumizi ya AI katika mazingira halisi.

Kampuni hiyo imesema kifaa hicho kinawezesha mawasiliano ya simu ya video kwa kutumia AI kwa pande zote, mawasiliano kwa kupitia lugha ya ishara ya mwili inayojieleza na mwendo wa mdundo. Pia hutoa ufanisi wa upigaji picha kwa kiwango cha sinema, ikiwemo mifumo ya kupiga picha za video za hali ya juu bila kutikisika na ufuatiliaji wa vitu inayoendeshwa na AI.

Kwenye tukio hilo, Honor ilitoa rasmi dhana ya AHI. "Msingi wa AI ni kutilia maanani watu," Li amesema. "Inapaswa kuchanganya akili ya ubongo (IQ) na akili ya kihisia (EQ), na kuongeza uwezo wa binadamu kubadilika kuendana na hali halisi, kujibadilisha ili kufurahia wakati uliopo katika dunia inayobadilika haraka. Hiyo ndiyo falsafa ya AHI ambayo Honor inaamini."

Siku hiyo hiyo, kampuni hiyo ya Honor pia ilizindua simu yake kinara inayokunjika, Magic V6, kwenye soko la kimataifa, ikiwa na unene wa kukunjika wa 8.75 mm. Roboti ya kwanza ya muundo wa binadamu ya kampuni hiyo pia imeonekana kwa mara ya kwanza kwenye tukio hilo.

Mkutano huo wa Simu za Mkononi wa Dunia kwa mwaka huu wa 2026 umeanza leo Machi 2 na utaendelea hadi Machi 5 mjini Barcelona, Hispania, huku sakafu yake ya maonyesho ikiwa na mabanda zaidi ya 100, yanayowakilisha nchi, maeneo na teknolojia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha