Usafiri wa treni za mizigo za China-Ulaya kwenye njia za mshariki wafikia mara zaidi ya 1,000 katika mwaka 2026 (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2026
Usafiri wa treni za mizigo za China-Ulaya kwenye njia za mshariki wafikia mara zaidi ya 1,000 katika mwaka 2026
Picha iliyopigwa Februari 26, 2026 ikionyesha treni za mizigo za China-Ulaya zikisubiri kuondoka kwenye Stesheni ya Reli ya Manzhouli katika Mji wa Manzhouli, Mkoa wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China. (Picha na Huang Xu/Xinhua)

Hadi kufikia Februari 26, 2026, usafiri wa treni za mizigo za China-Ulaya ulikuwa umefikia mara zaidi ya 1,000 kwenye njia zake za mashariki mwaka huu, ukivunja rekodi ya idadi hiyo siku 26 mapema kuliko mwaka jana.

Njia za mashariki za usafiri wa treni zinapita forodha tatu za reli za Manzhouli, Suifenhe na Tongjiang. Njia za uendeshaji wa treni zimepanuka hadi 27, zikifika miji zaidi ya 60 ya China na nchi 14 za Ulaya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha