Mji mdogo wa Taicang, China wakusanya kampuni zaidi ya 560 za Ujerumani kwa kiwango kipya cha uwekezaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 26, 2026
Mji mdogo wa Taicang, China wakusanya kampuni zaidi ya 560 za Ujerumani kwa kiwango kipya cha uwekezaji
Wateja wakiingia kwenye mgahawa wa Kijerumani mjini Taicang, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Februari 24, 2026. (Xinhua/Ji Chunpeng)

TAICANG –Taicang, yenye wakazi wake wa kudumu chini ya milioni moja, ni mji mdogo kwenye ukingo wa kusini wa mlango wa Mto Yangtze. Ukijulikana kama "maskani ya kampuni za Ujerumani" nchini China, mji huo wa Taicang hadi sasa umekusanya kampuni zaidi ya 560 zilizowekezwa kwa mtaji kutoka Ujerumani, tangu kampuni ya kwanza ya Ujerumani Kern-Liebers ilipoweka makao yake hapa mwaka 1993. Jumla ya uwekezaji wa aina hiyo imezidi dola bilioni sita za Marekani na thamani ya pato lao la viwanda la mwaka imezidi yuan zaidi bilioni 67 (dola za Marekani karibu bilioni 9.76).

Ilichukua miaka 14 kwa kampuni 100 za kwanza za Ujerumani kukusanyika Taicang, lakini miaka miwili tu kwa kampuni ya 400 hadi ya 500. Nyuma ya kasi hii ni matokeo ya mwongozo wa awali wa kila mara na uwezeshaji sahihi kwa miaka mingi wa serikali za mitaa.

Mji huo wa Taicang umekuwa ukihimiza kampuni za Ujerumani kuongeza uwekezaji na kupanua uzalishaji kwa kufanya matukio ya "Siku ya Taicang" nchini Ujerumani na kutoa njia rahisi kwa kampuni zinazowekezwa kwa mtaji kutoka Ujerumani. Eneo maalum la kwanza la viwanda la elimu ya ufundi ya mifumo miwili kati ya China na Ujerumani lililojengwa mjini Taicang limekuza vipaji zaidi ya elfu kumi vya kitaaluma vyenye ujuzi wa hali ya juu.

Mbali na ushirikiano wa kiviwanda, mabadilishano ya kati watu na watu wa China na Ujerumani pia yanazidi kuwa karibu zaidi katika mji huo wa Taicang. Mazingira ya maisha ya mtindo wa Kijerumani yanaweza kupatikana kwa urahisi hapa. Kanivali ya bia imekuwa ikifanyika Taicang kwa miongo miwili. Wajerumani wengi zaidi wanaoishi Taicang wanaweza kufurahia hisia ya kuwa nyumbani hapa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha