Lugha Nyingine
Soko la Wanunuzi la China lashuhudia mwanzo mzuri katika Mwaka Mpya wa Farasi (7)
| Watu wakiwa wamepanga foleni wakati wakisubiri kutazama filamu kwenye jumba la sinema katika Eneo la Xiqing la Mji wa Tianjin, kaskazini mwa China, Februari 20, 2026. (Xinhua/Li Ran) |
BEIJING - Soko la wanunuzi la China limepata mwanzo mzuri wakati wa likizo ya siku tisa ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi, ambayo imemalizika jana Jumatatu Februari 23, kwa matumizi kuongezeka maradufu hasa katika maeneo sita muhimu -- chakula, malazi, usafiri, utalii, manunuzi na burudani, ikiashiria mwanzo mzuri wa Mwaka Mpya wa Farasi.
Mamlaka za China zilianzisha mfululizo wa hatua za kisera ili kufungua nguvu bora za matumizi wakati wa likizo ya sikukuu hiyo, kwani mahitaji ya ndani yanabaki kuwa injini muhimu ya ukuaji wa uchumi. Serikali za mitaa za China zilitenga yuan bilioni 2.05 (dola za Marekani karibu milioni 295.23) katika ufadhili ili kunufaisha moja kwa moja umma kupitia vocha za matumizi, ruzuku na mgawanyo wa pesa taslimu wakati wa likizo hiyo.
Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi, ambayo ni sikukuu muhimu zaidi ya kijadi ya China, kwa kawaida huwa ni msimu wa kilele kwa matumizi ya wanunuzi, yakichochewa na mijumuiko ya familia, usafiri, ulaji wa vyakula, burudani na ununuzi wa zawadi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



