China yakadiria kushuhudia pilika nyingi za safari za abiria kurudi wakati likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya Wa Jadi ikimalizika (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 24, 2026
China yakadiria kushuhudia pilika nyingi za safari za abiria kurudi wakati likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya Wa Jadi ikimalizika
Abiria wakiwa wamepanga foleni ili kuingia katika Stesheni ya Reli ya Yinchuan mjini Yinchuan, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia, kaskazini magharibi mwa China, Februari 23, 2026. (Xinhua/Yang Zhisen)

Kundi la Kampuni za Shirika la Reli la China, ambalo ni mwendeshaji wa reli wa kitaifa wa China, limesema Jumatatu kwamba Februari 23, siku ya mwisho ya likizo ya siku tisa ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi, imekadiriwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kushuhudia pilika za idadi kubwa zaidi ya safari za abiria kurudi, na imetabiri kwamba safari milioni 18.5 zitafanywa kupitia mfumo wa reli katika siku hiyo.

Kundi hilo lilisema kwamba safari hizo zilizotarajiwa kufanywa jana Jumatatu zitafuata safari za abiria karibu milioni 18.3 zilizofanywa siku iliyotangulia ya Jumapili. Limeongeza kuwa, treni 2,297 za ziada zilikuwa zimepangwa kutoa huduma jana Jumatatu ili kukidhi mahitaji hayo makubwa ya usafiri.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha