Lugha Nyingine
Xu Mengtao wa China atetea ubingwa katika mchezo wa kuruka hewani kwa wanawake huko Milan-Cortina
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 19, 2026
LIVIGNO — Bingwa mtetezi wa Olimpiki kutoka China, Xu Mengtao, amehitimisha mara yake ya tano ya kushiriki kwenye Michezo ya Olimipiki ya Majira ya Baridi kwa kunyakua medali ya dhahabu siku ya Jumatano, akiwa bingwa wa mchezo wa kuteleza kwenye theluji kwa vitendo huria na kuruka hewani kwa wanawake (freestyle skiing women's aerials) katika Olimpiki ya Milan-Cortina.
Xu, mwenye umri wa miaka 35, alipata alama 112.90 na kujihakikishia ubingwa. Danielle Scott wa Australia alijinyakulia medali ya fedha kwa alama 102.17, huku Shao Qi wa China akishinda medali ya shaba kwa alama 101.90.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




