Kundi la kwanza la maduka ya bidhaa za kila siku yasiyotozwa ushuru kwa wakazi wa Hainan lafunguliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 13, 2026
Kundi la kwanza la maduka ya bidhaa za kila siku yasiyotozwa ushuru kwa wakazi wa Hainan lafunguliwa
Wateja wakichagua bidhaa kwenye duka la bidhaa za kila siku yasiyotozwa ushuru kwa wakazi wa kisiwa hicho mjini Haikou, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Februari 11, 2026. (Xinhua/Zhang Liyun)

Kundi la kwanza la maduka ya bidhaa za matumizi ya kila siku zisizotozwa ushuru kwa wakazi wa kisiwani katika Mkoa wa Hainan, kusini mwa China limefunguliwa rasmi jana Jumatano. Usambazaji wa maduka hayo matano ya kwanza ya bidhaa za matumizi ya kila siku zisizotozwa ushuru ni matatu katika Mji wa Haikou, moja katika Mji wa Sanya, na moja katika Mji wa Danzhou.

Kwa mujibu wa taratibu zilizotolewa na mamlaka husika, kila mkazi anayestahiki anapewa mgao wa manunuzi ya mwaka ya bidhaa zisiyotozwa ushuru wa yuan 10,000 (dola za Marekani takribani 1,437), bila kikomo katika idadi ya manunuzi. Sera hiyo inahusu mahitaji ya kila siku, ikiwemo chakula na vinywaji maalum, bidhaa za kemikali za matumizi ya kila siku, bidhaa za nyumbani, na vitu vya akina mama wajawazito na watoto.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha