Lugha Nyingine
Maonesho ya umeme wa jua ya Afrika yafunguliwa nchini Kenya (7)
![]() |
| (Xinhua/Xie Jianfei) |
Maonesho ya Umeme wa Jua Afrika "Intersolar Africa 2026" yamefunguliwa Jumanne jijini Nairobi, nchini Kenya, yakiwavutia zaidi ya waoneshaji 100 wa kikanda na wa kimataifa kuonesha teknolojia zinazowezesha mpito wa kuelekea uchumi wa kijani barani Afrika.
Maafisa waandamizi wa serikali, watendaji wa sekta hiyo, na wavumbuzi walihudhuria sherehe ya ufunguzi wa maonesho hayo na mkutano mkuu wa Afrika Mashariki kuhusu umeme wa jua na uhifadhi wa nishati, ambao uliendelea hadi Jumatano.
Katibu mkuu katika Wizara ya Nishati na Petroli ya Kenya, Alex Wachira, amesema teknolojia za nishati ya jua zimeharakisha mpito wa kuelekea uchumi wa kijani barani Afrika, huku zikiongeza ustahimilivu wa tabianchi na ukuaji jumuishi.
Naye mkurugenzi wa mikakati wa Baraza la Umeme wa Jua Duniani, Alyssa Pek, alisema Afrika imeibuka kama moja ya masoko ya kimkakati zaidi kwa bidhaa za nishati ya jua, ikichochewa na hitaji la kufikia malengo ya utoaji kaboni sifuri na Malengo ya Maendeleo Endelevu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa, Gerd Muller, amesema katika ujumbe wa video kwamba rasilimali kubwa za nishati ya jua barani Afrika zinapaswa kutumika kuchochea ukuaji, kufungua viwanda, na kuleta ajira.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




