Mfanyakazi wa matengenezo ya treni za mwendo-kasi alinda usalama wa pilika za usafiri wa likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 05, 2026
Mfanyakazi wa matengenezo ya treni za mwendo-kasi alinda usalama wa pilika za usafiri wa likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Li Qiwei akifanya kazi ndani ya ghala ya matengenezo ya treni za mwendo-kasi katika Mji wa Tianjin, kaskazini mwa China, Februari 1, 2026. (Xinhua/Zhao Zishuo)

TIANJIN - Treni kadhaa za Mwendo-Kasi zilikuwa zimepangwa vizuri kwa ajili ya "ukaguzi wa afya" ndani ya ghala ya matengenezo katika Mji wa Tianjin usiku wa Februari 1, muda mfupi tu kabla ya kuanza kwa pilika za mwaka huu za usafiri wa likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, safari ya kila mwaka ya watu kurudi nyumbani nchini China, na pia usafiri wa watu wengi zaidi duniani.

Ili kuhakikisha treni hizo zinaondoka salama na kwa wakati, Li Qiwei, kiongozi wa timu ya matengenezo, alilazimika kufanya kazi usiku kucha na wafanyakazi wenzake zaidi ya 40 ili kufanya ukaguzi kamili wa seti 28 za Treni za Mwendo-Kasi -- mzigo wa kazi ambao ni mkubwa kwa asilimia karibu 20 kuliko ule wa siku ya kawaida ya kazi.

Li amekuwa akifanya kazi kwenye ghala hiyo ya matengenezo baada ya kuhitimu shahada ya uhandisi wa vyombo vya usafiri kutoka Chuo Kikuu cha Dalian Jiaotong. Miaka minane ya bidii imeshuhudia akipanda ngazi za vyeo kutoka kuwa mfanyakazi wa kawaida hadi kuwa kiongozi wa kikundi mwenye uwezo.

Amesema anahisi kuwa mwenye bahati sana kuweza kuchangia katika uendeshaji salama wa treni za mwendo-kasi, ambao husaidia mamilioni ya watu kujumuika na familia zao wakati wa pilika za usafiri wa likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha