Lugha Nyingine
Wanafunzi wa kigeni wakumbatia furaha ya sherehe ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China katika Mji wa Chongqing
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 04, 2026
Wakati sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ikikaribia kuwadia, Eneo la Banan la Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China limeandaa shughuli ya "Laowai@Chongqing". "Laowai" ni neno la lugha ya Kichina maana yake ni "raia wa kigeni".
Wanafunzi ishirini waliotoka nchi mbalimbali walikusanyika pamoja ili kushiriki kwenye shughuli changamani za mila na desturi za kitamaduni za wenyeji wa huko, wakiimba nyimbo za kienyeji za Mudong, kutengeneza sanaa ya kukata karatasi, na kutengeneza keki za wali wa kunata, wamekumbatia mazingira ya sherehe ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ambayo itakuwa Februari 17 mwaka huu.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




