China na ASEAN zasaini makubaliano ya toleo mpya ya FTA ili kuhimiza ushirikiano wa ngazi ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 29, 2025
China na ASEAN zasaini makubaliano ya toleo mpya ya FTA ili kuhimiza ushirikiano wa ngazi ya juu
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria Mkutano wa 28 wa China na Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) mjini Kuala Lumpur, Malaysia, Oktoba 28, 2025. (Xinhua/Li Xiang)

KUALA LUMPUR - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema mjini Kuala Lumpur, Malaysia jana Jumanne kwamba makubaliano mapya yaliyosainiwa ya Eneo la Biashara Huria la China na ASEAN (CAFTA) toleo la 3.0 yanaonyesha fursa mpya ya kupanua na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili wa uchumi na biashara.

Li amesema hayo kwenye Mkutano wa 28 kati ya China na Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) uliofanyika Kuala Lumpur jana Jumanne asubuhi. Kabla ya mkutano huo, Li na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim walishuhudia kusainiwa kwa Itifaki ya toleo la 3.0 ya CAFTA.

Kwenye hafla hiyo ya utiaji saini, wakiwa na bendera za taifa za China na nchi wanachama wa ASEAN nyuma yao, Waziri wa Biashara wa China Wang Wentao na Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Malaysia Tengku Zafrul Abdul Aziz walitia saini nyaraka zao husika wakiwa wameshuhudiwa na Waziri Mkuu Li na Waziri Mkuu Anwar. Kisha waziri huyo wa Malaysia aliwasilisha nyaraka hiyo kwa Katibu Mkuu wa ASEAN Kao Kim Hourn.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha