Lugha Nyingine
Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano wa China waipa uchumi halisi kipaumbele
Uchumi wa China utaendeleaje katika kipindi chake cha Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano (2026-2030)?
Mkutano wa nne wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China umepanga majukumu 12 ya kimkakati kwa maendeleo ya uchumi na jamii katika kipindi hicho, huku “kujenga mfumo wa viwanda vya mambo ya kisasa, kuimarisha na kupanua msingi wa uchumi halisi (real economy)” kumewekwa kwenye nafasi ya kwanza, hali ambayo imethibitisha umuhimu wa uchumi halisi.
"Uchumi halisi ni msingi wa nchi kubwa." Kwa hivi sasa hali ya kimataifa ni ngumu na yenye utatanishi, na umuhimu wa uchumi halisi umedhihirika zaidi.
Kwa namna gani China itaimarisha uchumi halisi ukiwa kama “msingi wa kuanzishwa kwa nchi na kuimarishwa kwa nguvu ya nchi?” Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wiki iliyopita, Zheng Shanjie, ambaye ni mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China alitoa ufafanuzi kuhusu hilo. Alisema, majukumu makubwa yanahusu pande nne zinazofuata:
Kuimarisha yaliyopo na kuyaboresha katika kuendeleza viwanda vya jadi. Viwanda vya jadi vya China ni vyenye ukubwa zaidi, vikiwa msingi wa mfumo wa hivi sasa wa viwanda vya China na kuchukua zaidi ya 80% ya sekta ya viwanda vya utengenezaji wa bidhaa. Katika kipindi cha mpango wa 15 wa miaka mitano ya maendeleo, China itaongeza nafasi ya soko la fedha za yuan trilioni 10 hivi ndani ya miaka mitano ijayo kwa kupitia kuhimiza uboreshaji wa viwanda muhimu.
Kuvumbua na kuhimiza uvumbuzi katika kuandaa na kuendeleza viwanda vipya na viwanda vya siku za baadaye. Katika kipindi cha mpango huo, China itajenga viwanda vipya vilivyo vya nguzo, kuharakisha kukusanyika kwa viwanda vipya kama vile vya nishati mpya na nyenzo mpya, kupanga kwa mtazamo wa muda mrefu viwanda vya siku za baadaye kama vile vya teknolojia ya kwanta, utengenezaji wa bidhaa za kibaiolojia, n.k. Ukubwa wa viwanda vitakavyoongezwa katika miaka 10 ijayo utakuwa sawa sawa na kuanzishwa kwa viwanda vingine vya teknolojia ya hali ya juu nchini China.
Kuongeza uwezo na ubora na kuhimiza maendeleo yenye ufanisi wa juu ya shughuli za huduma. China itachukua hatua za kuongeza uwezo na ubora wa shughuli za huduma, kuinua kiwango cha mafungamano ya maendeleo ya shughuli za huduma za mambo ya kisasa, viwanda vya utengenezaji wa kisasa na kilimo cha kisasa, ili kukidhi vizuri zaidi mahitaji ya watu juu ya maisha mazuri na kuleta nafasi mpya kwa ongezeko la uchumi.
Kuimarisha msingi na kuongeza ufanisi, na kuharakisha kujenga mfumo wa miundombinu wa mambo ya kisasa. China itaimarisha mpango wa jumla kuhusu miundombinu, kupanga kwa mapema kiasi cha kufaa ujenzi wa miundombinu ya aina mpya, kuhimiza vizuri zaidi mafungamano ya mawasiliano, uratibu na maendeleo salama yenye ufanisi wa juu ya miundombinu.
Uchumi wa China ulipata mafanikio yake kuanzia uchumi halisi, na pia utaelekea siku za baadaye kwa kutegemea uchumi halisi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




