

Lugha Nyingine
Sehemu ya Anhui ya Mradi wa Usambazaji Umeme wa Volti ya Juu wa Gansu-Zhejiang yaingia kipindi cha kufunga waya (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 17, 2025
![]() |
Picha iliyopigwa Septemba 16, 2025 ikionesha wafanyakazi wakifunga waya kwa Mradi wa Usambazaji Umeme wa volti ya juu ya ±800 kV (UHV) wa moja kwa moja wa Gansu-Zhejiang katika Wilaya ya Nanling, Wuhu, Mkoa wa Anhui wa Mashariki mwa China. (Xinhua/Liu Junxi) |
Sehemu ya Anhui ya Mradi wa Usambazaji Umeme wa volti ya juu ya ±800 kV (UHV) wa moja kwa moja wa Gansu-Zhejiang, unaounganisha Mkoa wa Gansu wa Kaskazini Magharibi mwa China na Mkoa wa Zhejiang wa Mashariki mwa China, hivi karibuni imeingia kwenye kipindi cha kufunga waya wa umeme.
Njia hiyo ya kusafirisha umeme yenye urefu wa kilomita 2,370 inaanzia Wuwei, Gansu na kuendelea hadi Shaoxing, Zhejiang. Baada ya kuzinduliwa kwake, njia hiyo itasaidia usafirishaji wa nishati safi kutoka Kaskazini Magharibi mwa China na kupunguza hali ya upungufu wa nishati katika Mashariki mwa China.
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma