Kikosi cha manowari cha China kikiongozwa na Manowari ya kubeba ndege za kivita Shandong chatembelea Hong Kong (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2025
Kikosi cha manowari cha China kikiongozwa na Manowari ya kubeba ndege za kivita Shandong chatembelea Hong Kong
Waandishi wa habari kwenye nyanda za juu wakichukua picha za kikosi cha manowari za Jeshi la Majini la Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) zikiongozwa na manowari Shandong kilipowasili Hong Kong, kusini mwa China, Julai 3, 2025.(Xinhua/Chen Duo)

HONG KONG - Katika siku yake ya kuzaliwa kufikisha miaka 28, Luteni Xie Huigui wa Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) alikuwa ndani ya manowari ya kubeba ndege za kivita, Shandong iliyoundwa kwa kujitegemea na China, ambayo yuko ziara ya siku tano katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR).

Alizaliwa Julai 1, 1997, siku ya kurudi kwa Hong Kong katika nchi mama. Jina lake alilopewa "Huigui" -- linalomaanisha "kurudi" -- liliadhimisha siku hiyo ya kihistoria.

Xie amewasili Hong Kong jana Alhamisi asubuhi akiwa amepanda manowari hiyo Shandong. Manowari hiyo ya kubeba ndege za kivita, ikiongoza kikosi chenye kujumuisha manowari nyingine tatu, iliingia Bandari ya Victoria saa 2 asubuhi.

Kikosi hicho cha manowari kilisindikizwa na helikopta na meli zilizotumwa na serikali ya Hong Kong na Kikosi cha Hong Kong cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) ambapo zaidi ya maafisa na wanajeshi 700 walijipanga kwa maneno ya kichina "nchi salama, nyumbani pazuri" kwenye sitaha ya manowari hiyo Shandong.

"Ninajihisi mwenye bahati sana kuweza kuiona manowari Shandong kwa macho yangu mwenyewe. Inapendeza sana," rubani mstaafu wa baharini amesema akitazama manowari hizo kwa darubini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha