Fundi wa kutengeneza kahawa wa China ashinda taji la ubingwa katika WBC 2025 (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2025
Fundi wa kutengeneza kahawa wa China ashinda taji la ubingwa katika WBC 2025
Fundi wa kutengeneza kahawa (Barista) wa China Peng Jinyang akishiriki kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Watengenezaji Kahawa (WBC) 2025 mjini Jakarta, Indonesia, Mei 15, 2025. (Xinhua)

Peng Jinyang, fundi wa kutengeneza kahawa (Barista) na mmiliki wa duka la kahawa la Captain George mjini Guiyang, China hivi majuzi alishinda taji la ubingwa katika Kombe la Dunia la Watengenezaji Kahawa (WBC) nchini Indonesia 2025.

Aliona kwamba chini ya mazingira sawa, hata kama vikombe vitatu vya kahawa vingetengenezwa kwa mfululizo, kusingekuwa na tofauti ndogo ndogo katika ladha ya kila kikombe.

Ustadi wake unatokana na miaka mingi ya kusafisha kaakaa lake, ambapo kupitia hilo aligundua jinsi mabadiliko ya halijoto kati ya spout na sehemu ya katikati ya sufuria ya kahawa inavyoathiri ladha. Hii ikawa mada ya hotuba yake katika WBC, ambayo ilipata sifa kubwa kutoka kwa majaji.

Mwaka 2012, Peng, wakati huo akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye kuvutiwa na ladha tajiri kutokana na kukaangwa kwa buni, alianzisha duka la kahawa na barista mwenzake mjini Guiyang. Wakati huo, habari za kahawa za nyumbani zilikuwa chache, na aina za buni zilikuwa kidogo. Kwa msaada wa wazazi wake, alinunua mashine ya kukaanga buni na kujifunza jinsi ya kukaanga kutokana na video za lugha ya Kiingereza.

Ili kuongeza ustadi wake, alihudhuria semina za kahawa sehemu mbalimbali za China na mwaka 2019, alianza kualika mabingwa wa kahawa duniani kutoa mafunzo mjini Guiyang. Kwa utaalam wake, Peng alitwaa tuzo ya bingwa katika Mashindano ya Kimataifa ya Kahawa ya TAKAO mwaka 2016, na kuwa nahodha wa kuiongoza timu yake kushinda taji la ubingwa wa WBC wa China kwa miaka minne mfululizo tangu 2022.

"Kuleta mabingwa hawa ni muhimu kwa kupata maarifa ya hivi punde ya kahawa na kuhakikisha kuwa mabarista wa Guiyang, licha ya kuwa ni mji ulio ndani ya bara, wanakuwa katika mstari wa mbele kwenye mambo ya kahawa," Peng alisema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha