

Lugha Nyingine
Wataalam wasisitiza umuhimu wa kimataifa wa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China katika Baraza la Hong Ting mjini Cairo (7)
![]() |
Liao Liqiang, Balozi wa China nchini Misri na mwakilishi kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiarabu akihutubia shughuli iliyopewa jina la "Mazungumzo ya Cairo ya Baraza la Hong Ting: Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China, Uzoefu Wenye Thamani kwa Dunia" mjini Cairo, Misri, Aprili 24, 2025. (Xinhua/Sui Xiankai) |
CAIRO – Ujenzi wa mambo ya kisasa wa China si tu kwamba unaboresha maisha ya watu wa China lakini pia unatoa fursa za maendeleo za pamoja duniani kote, haswa kwa nchi zinazoendelea, wataalam wamesema kwenye "Mazungumzo ya Cairo yaBaraza la Hong Ting: Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China, Uzoefu Wenye Thamani kwa Dunia" yaliyofanyika katika mji mkuu wa Misri jana Alhamisi.
Shughuli hiyo, iliwakutanisha wawakilishi zaidi ya 100 kutoka Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, serikali ya China na Misri, taasisi za washauri bingwa, vyombo vya habari, na sekta binafsi.
Baraza hilo lilianza kwa kipindi cha ufunguzi ambapo washiriki waliangazia mikakati shirikishi ya kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa na kuharakisha maendeleo ya jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja.
Kipindi hicho kilifuatiwa na vipindi viwili vya mazungumzo vilivyoongozwa na wataalam vikishirikisha wawakilishi kutoka vyombo vya habari na taasisi za washauri bingwa. Wakati wa majadiliano hayo, washiriki walibadilishana maoni kuhusu umuhimu wa kimataifa wa njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China na kuchambua mchango wake kutoka kwa mtazamo wa Nchi za Kusini, wakisisitiza umuhimu wake kwa nchi zinazoendelea.
Katika hotuba yake kwenye kipindi cha ufunguzi, Waziri Mkuu wa zamani wa Misri, Essam Sharaf amesema kuwa China imepata ustawi wa ndani kupitia ujenzi wa mambo ya kisasa na inatoa mchango kwa ajili ya ustawi wa dunia kwa kuhimiza jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
"Maendeleo ya China inaimarisha nguvu za kimataifa ya amani na maendeleo. Ujenzi wa mambo ya kisasa wa China umekuwa fursa muhimu kwa maendeleo ya dunia," amesema Liao Liqiang, Balozi wa China nchini Misri ambaye pia ni mwakilishi wa China kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.
Balozi huyo wa China amesisitiza kwamba katika kukabiliana na ukadamizaji wa ushuru, China imeshikilia msimamo wake si tu kulinda haki na maslahi yake halali bali pia kulinda maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa -- hasa nchi nyingi zinazooendelea -- na kudumisha haki na usawa duniani.
Ameongeza kuwa, China na nchi za Kiarabu zinatazamiwa kupiga hatua zaidi kupitia ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na juhudi za pamoja za ujenzi wa mambo ya kisasa, zikigeuza mivutano ya sasa ya biashara ya kimataifa kuwa fursa mpya za ushirikiano.
Mkurugenzi wa Baraza la Misri kwa Mambo ya Nje Ezzat Saad amesema kuwa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China unavunja imani potofu kwamba ujenzi wa mambo ya kisasa lazima ufuate njia ya Magharibi, akisema kuwa mtindo wa China unatoa njia mbadala kwa nchi zinazoendelea na unatoa mchango kwa ajili ya maisha ya kisasa ya binadamu wote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma