Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-20 cha China chaunganishwa na kituo cha anga ya juu cha China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2025
Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-20 cha China chaunganishwa na kituo cha anga ya juu cha China
Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing Aprili 24, 2025 ikionyesha wanaanga wa chombo cha Shenzhou-19 wakijiandaa kuwakaribisha wanaanga wa chombo cha Shenzhou-20. (Xinhua/Jin Liwang)

BEIJING – Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limesema kuwa, Chombo cha anga ya juu cha China cha Shenzhou-20 kilichorushwa mapema jana Alhamisi jioni kimeunganishwa pamoja kwa mafanikio na kituo cha anga ya juu cha China usiku wa jana Alhamisi.

Chombo hicho cha anga ya juu kilifanya mijongeo nyumbulifu ya haraka na ya kiotomatiki kikiunganishwa na sehemu ya radial ya chombo kikuu cha Tianhe cha kituo cha anga ya juu cha China, saa 5:49 usiku (saa za Beijing). Mchakato mzima ulichukua saa takriban 6.5, imesema CMSA.

Mapema leo Ijumaa asubuhi Shirika la CMSA limesema, baada ya kuunganishwa na kituo cha anga ya juu cha China wanaanga hao watatu waliokuwa ndani ya chombo hicho walianza kufanya mchakato wa kuingia kwenye chombo kikuu cha Tianhe, wameingia kwa mafanikio na kupokelewa na wanaanga wa chombo cha Shenzhou-19 ambao wamekuwa kwenye anga ya juu tangu walipopelekwa Oktoba 30 mwaka jana.

Chombo hicho kilicho juu ya roketi ya kubeba ya Long March-2F, kimerushwa kutoka Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Jiuquan kaskazini magharibi mwa China mapema jana Alhamisi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha