Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na mwenzake wa Kenya William Ruto (3)

(CRI Online) April 24, 2025
Rais Xi Jinping afanya mazungumzo na mwenzake wa Kenya William Ruto
(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping leo asubuhi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Kenya William Ruto ambaye yuko ziarani nchini China katika Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing. Wakuu hao wawili wamekubaliana kuinua uhusiano wa nchi hizo mbili hadi kufikia ngazi ya Jumuiya ya China na Kenya yenye Mustakbali wa Pamoja katika Zama Mpya.

Rais Xi amebainisha kuwa, kuinuka kwa uhusiano kati ya China na Kenya ni chaguo la kimkakati la pande mbili. China inapenda kushirikiana na na Kenya, zikifuata mkondo wa historia na mwelekeo wa zama, kuweka mfano wa Jumuiya yenye mustakbali wa pamoja kati ya China na Afrika kwa hali zote katika zama mpya, na kuongoza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika na umoja na ushirikiano kati ya nchi za Kusini mwa Dunia.

Rais Ruto amesema ushirikiano kati ya China na Afrika unasaidia amani na maendeleo ya Afrika, Kenya inapenda kuimarisha uratibu na China, na kutekeleza vyema matokeo yaliyopatikana katika Mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Amesisitiza kuwa Kenya inapongeza China kwa kufanya kazi kama kitulizi katika mazingira ya sasa ya kimataifa yenye sintofahamu na mitikisiko, na kulinda maslahi halali ya nchi za Kusini mwa Dunia. Amesema Kenya inapenda kushirikiana na China katika kulinda na kutekeleza mifumo ya pande nyingi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha