Ujenzi wa Mfereji wa Pinglu katika Mkoa wa Guangxi, China waonyesha maendeleo makubwa (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2025
Ujenzi wa Mfereji wa Pinglu katika Mkoa wa Guangxi, China waonyesha maendeleo makubwa
Picha iliyopigwa Novemba 12, 2025 ikionyesha eneo la ujenzi wa kituo cha Madao kwenye Mfereji wa Pinglu mjini Qinzhou, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhou Hua)

Miaka mitatu baada ya kuanza kwa ujenzi, Mfereji wa Pinglu katika Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, ambao ni sehemu muhimu ya Ushoroba Mpya wa Biashara ya Kimataifa ya Baharini na Nchi Kavu umeonyesha maendeleo makubwa.

Utakapokamilika, mfereji huo wenye urefu wa kilomita 134.2 utapitia miji ya Nanning na Qinzhou ya mkoa huo wa Guangxi hadi kufikia Ghuba ya Beibu. Unatarajiwa kuwa njia muhimu ya usafiri wa pamoja wa bahari na mto katika eneo la kusini-magharibi mwa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha