Lugha Nyingine
Safari za abiria kwa reli nchini China zafikia rekodi mpya katika miezi 11 ya kwanza mwaka 2025 (4)
![]() |
| Picha iliyopigwa Agosti 17, 2025 ikionyesha treni ya mwendokasi ikiendeshwa kwenye reli ya Harbin-Qiqihar. (Picha na Yuan Yong/Xinhua) |
BEIJING - Takwimu zilizotolewa jumanne na Kundi la Kampuni za Reli la China zimeonyesha kuwa, mtandao wa reli wa China umehudumia idadi ya safari za abiria inayovunja rekodi katika miezi 11 ya kwanza ya 2025, na katika kipindi hicho cha Januari hadi Novemba, idadi ya safari za abiria kwa reli ilifikia bilioni 4.28 kote nchini, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.6 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Wastani wa treni 11,258 za abiria ziliendeshwa kwa siku katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.1 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, kampuni hiyo imesema.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, ili kuongeza matumizi ya huduma, huduma maalum za treni zilianzishwa ili kukidhi mahitaji ya usafiri yaliyochochewa na matukio ya maeneo husika kama vile mashindano ya michezo, maonyesho na burudani.
Kampuni hiyo imesema kuwa, usafiri wa abiria wa kuvuka mipaka pia ulishika kasi, huku Njia ya Reli ya kasi ya Guangzhou-Shenzhen-Hong Kong na Reli ya China-Laos zikihudumia safari za abiria wa kuvuka mipaka milioni 28.94 na 244,000 mtawalia katika kipindi hicho.
Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo imeeleza kuwa, kuanzia Januari hadi Novemba, uwekezaji wa mali isiyohamishika katika sekta ya reli ya China uliongezeka kwa asilimia 5.9 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




