Lugha Nyingine
Bustani kubwa zaidi duniani ya mandhari ya barafu na theluji yafunguliwa, ikichochea shauku ya utalii wa majira ya baridi wa China (5)
HARBIN – Majira ya saa 4 asubuhi, jana Jumatano Bustani maarufu zaidi ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin katika Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China ilifunguliwa rasmi katika majira ya baridi nchi hiyo ya mwaka huu, ikionesha bustani hiyo ya aina mpya ya kuvutia zaidi hadi sasa, ambapo vivutio vya alama, huduma za ipasavyo na sanaa za kuchonga za barafu kwenye eneo la bustani lenye ukubwa wenye kuvunja rekodi wa mita za mraba milioni 1.2.
He Rui akikabiliwa na upepo mkali anateleza kwenda chini kwenye Vitelezi vya Barafu vyenye urefu wa Mita 521 katika bustani hiyo, wakati kundi la kwanza la watalii wa majira ya baridi ya mwaka huu walipomiminika kwenye bustani hiyo kubwa zaidi ya mandhari ya barafu na theluji duniani siku hiyo ya Jumatano, kwa ajili ya burudani ya majira ya baridi ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.
Mtalii huyo kutoka Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China amesafiri kilomita zaidi ya 3,000 kwa ajili ya kujiburudisha katika utalii huo wa maajabu baada ya kutarajia kwa miaka mingi, na alionekana kufurahishwa kwelikweli na burudani hiyo ya kusisimua.
Kama ilivyo kwa mtalii huyo He, watembeleaji wengi wa mapema walikimbilia kwenye vivutio vya alama vya bustani hiyo na walifurahishwa na mazingira yaliyoboreshwa.
Guo Hongwei, mwenyekiti wa Kampuni ya Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin amesema Vitelezi vya Barafu vimedumisha mpangilio wake wa leni 24 na kupanua njia yake ndefu zaidi ya kuteleza hadi kufikia mita 521, huku gurudumu kubwa la angani la mita 120 pia likifunguliwa tena, na kuwapa wageni uangaliaji wa kutoka juu wa kila maajabu ya majira ya baridi kwenye bustani hiyo.
Kwenye lango la bustani hiyo, kuna maonesho ya densi na ngoma, pamoja na makopo ya "Barafu ya Siku-ya kwanza," yalitolewa maalum ili kukaribisha watembeleaji wa mapema. Barafu hiyo iliyokusanywa wakati wa tamasha la awali la kukata barafu la Harbin, inaashiria bahati nzuri katika desturi za wenyeji na haraka ikawa mada inayofuatiliwa na kuvuma kwenye mitandao ya kijamii ya China.
Mnara mkuu ni jengo refu na kubwa zaidi katika bustani hiyo, umeumbwa kama neno‘mlima’la Kichina, ‘mlima’ ambao ulifunikwa na theluji, ikiashiria matarajio ya nchi kwa ustawi wa uchumi wa barafu na theluji.
Sanaa za kuchonga za barafu za mwaka huu zinaonyesha mafungamano ya kuvutia ya maajabu ya Dunia nzima ya kihistoria na ya zama za hivi sasa.
"Tumejitolea kuwapa watembeleaji kanivali kubwa ya barafu na theluji kwa kutumia rasilimali zetu za majira ya baridi na huduma zinazoboreshwa kila wakati," Guo ameongeza.
Mji wa Harbin, unaoitwa "mji wa barafu" wa China, umegeuza majira yake ya baridi ya muda mrefu zaidi kuwa majira muhimu yenye vivutio vya utalii. Katika majira ya baridi ya mwaka jana, mji mkuu huo wa Mkoa wa Heilongjiang ulikaribisha wageni milioni 90.36 walio wa rekodi mpya , na kupata mapato ya yuan bilioni 137.22 (dola za Marekani takribani bilioni 19.44), ongezeko la asilimia 16.6 ikilinganishwa majira ya baridi ya mwaka uliotangulia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




