Mwonekano wa madaraja mbalimbali ya Guizhou, China, "makumbusho ya madaraja duniani” (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2025
Mwonekano wa madaraja mbalimbali ya Guizhou, China,
Picha hii iliyopigwa Agosti 9, 2018 ikionyesha Daraja la Beipanjiang katika Mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa China (Xinhua/Ou Dongqu)

Guizhou, mkoa pekee usio na ardhi tambarare hata moja nchini China, hali ya jumla ya ardhi yake ni ya mabonde ya kina kirefu, kwa muda mrefu umekuwa ukitegemea mahandaki na madaraja ili kushinda mazingira yake magumu ya magenge yenye miamba.

Tangu mwaka 2012, mkoa huo umeharakisha juhudi zake za ujenzi wa madaraja. Mkoa huo wa Guizhou sasa una madaraja zaidi ya 32,000 ambayo ama tayari yamekamilika kujengwa au yanaendelea kujengwa - ongezeko kwa mara kumi ikilinganishwa na miaka ya 1980.

Kwa sababu ya idadi yake kubwa ya madaraja, aina mbalimbali za madaraja na teknolojia ngumu za ujenzi, mkoa huo Guizhou umepata jina la "makumbusho ya madaraja ya duniani."

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha