Lengshui wa Chongqing, China waendeleza utalii wa mapumziko wa kutazama mandhari ili kuhimiza sekta ya utalii (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 15, 2025
Lengshui wa Chongqing, China waendeleza utalii wa mapumziko wa kutazama mandhari ili kuhimiza sekta ya utalii
Picha iliyopigwa Desemba 13, 2025 ikionyesha barabara kuu inayopita milimani katika Tarafa ya Lengshui, Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Watujia ya Shizhu, Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China (Xinhua/Tang Yi)

Tarafa ya Lengshui katika Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Watujia ya Shizhu, Mji wa Chongqing, kusini magharibi mwa China, iliyo kwenye mwinuko wa wastani wa mita takriban 1,400 kutoka usawa wa bahari na kiwango cha ufunikaji wa misitu cha asilimia takriban 85, ina utajiri wa rasilimali za ikolojia. Katika miaka ya hivi karibuni, tarafa hiyo imejenga hoteli ndogo za wageni zenye usanifu maalum, na kuendeleza utalii wa mapumziko na kutazama mandhari, ikitumia kwa ufanisi rasilimali za vijijini na kuchochea maendeleo ya sekta ya utalii.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha