Kituo Kipya cha Uhifadhi na Utafiti wa Panda chaanza kufanya kazi kwa majaribio kusini mwa China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 05, 2025
Kituo Kipya cha Uhifadhi na Utafiti wa Panda chaanza kufanya kazi kwa majaribio kusini mwa China
Mhifadhi akimlisha panda kwenye Kituo cha Mianyang cha Uhifadhi na Utafiti wa wa Panda cha China katika Mji wa Mianyang, Mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China, Novemba 4, 2025. (Xinhua)

Kituo cha Mianyang cha Taasisi ya Uhifadhi na Utafiti wa Panda ya China, ambacho kilijengwa kwa muda wa miaka mitatu kimeanza kufanya kazi kwa majaribio jana Jumanne huko Mianyang, Mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China. Panda kumi na tatu kutoka vituo vya Wolong Shenshuping na Dujiangyan vya Taasisi ya Uhifadhi na Utafiti wa Panda ya China wamehamia kwenye makazi yao mapya katika kituo hiki kipya cha Mianyang kilichofunguliwa siku hiyo.

Kituo cha panda cha Mianyang, kina ukubwa wa hekta takriban 120, kituo hiki kiko kwenye bustani ya kiikolojia katika Mji wa Mianyang. Katika kituo hiki kuna sehemu za panda zaidi ya 50, na mazingira ya sehemu hizo ni mazuri na yanakidhi mahitaji ya kuzaliana kwa panda.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha