Lugha Nyingine
Ofisa Mwandamizi wa Umoja wa Mataifa asikitika kutojali kuhusu ukatili nchini Sudan (3)
![]() |
| Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia mambo ya ubinadamu wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Oktoba 30, 2025. (Manuel Elias/Picha ya UN/ kupitia Xinhua) |
UMOJA WA MATAIFA - Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia mambo ya ubinadamu na uratibu wa msaada wa dharura wa Umoja wa Mataifa Bw.Tom Fletcher ameeleza masikitiko kuhusu jumuiya ya kimataifa kupuuza ukatili nchini Sudan.
Jana Alhamisi Fletcher ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: "El Fasher -- tayari limekuwa eneo la majanga ya mateso ya binadamu -- limeingia katika jehanamu nyeusi zaidi, huku kukiwa na ripoti za kuaminika za mauaji yaliyoenea baada ya wapiganaji wa Vikosi vya Uungaji Mkono wa Haraka kuingia katika mji huo."
Amesema, wanawake na mabinti wanabakwa, watu wanakatwa viungo na kuuawa -- bila kujali kabisa. Ameeleza kuwa, juzi Jumatano, wagonjwa karibu 500 na wenzao wanaowatunza katika Hospitali ya Uzazi ya Saudi Arabia huko El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, waliripotiwa kuuawa.
Amesema, makumi ya maelfu ya raia wenye hofu na njaa kali wamekimbia au wako wanakimbia. Na wale wanaoweza kukimbia – wengi wao, ni wanawake, watoto, na wazee -- wanakabiliwa na unyang'anyi, kubakwa na ukatili katika safari hatari. Amesema, vijana wametekwa nyara au kuuawa barabarani na idadi kubwa ya watu wamezuiliwa kuondoka katika eneo hilo.
"Kinachoendelea huko El Fasher kinawafanya watu kukumbuka hofu kubwa ya mateso iliyoikumba Darfur miaka 20 iliyopita. Lakini kwa namna fulani leo tunaona mwitikio tofauti sana wa jumuiya ya kimataifa -- wa kujiweka pembeni. Kwa hiyo huu pia ni msukosuko wa upuuzi mkali," amesema.
Ametoa wito kwa Baraza la Usalama na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuchukua mara moja hatua zenye nguvu kubwa za kukomesha ukatili huo dhidi ya raia na kuacha kuwezesha kwa silaha vurugu hizo, na ameomba ufikiaji kamili na usiozuiliwa wa msaada wa ubinadamu huko El Fasher na kila mahali nchini Sudan.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




