Lugha Nyingine
Uwanja wa Ndege wa Guangzhou Baiyun, China wazindua T3 na njia ya tano ya ndege kurukia na kutua (3)
GUANGZHOU - Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou Baiyun mjini Guangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, jana Alhamisi umezindua rasmi Kituo chake cha 3, T3 na njia ya tano ya ndege kurukia na kutua, ikiufanya kuwa uwanja wa ndege wa kwanza wa kiraia wa China kuendesha njia tano za kurukia na kutua ndege za kibiashara.
Upanuzi wa Uwanja huo wa ndege, moja ya vituo vitatu vikubwa zaidi vya usafiri wa anga vya nchi hiyo, ni hatua nyingine kuelekea kujenga kundi la viwanja vya ndege vyenye kiwango cha dunia katika Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka husika za uwanja huo, katika siku za baadaye, uwanja huo wa ndege utaweza kuhudumia abiria milioni 120 na tani milioni 3.8 za mizigo na vifurushi. Aidha, ukiwa na vituo vyenye uwezo wa kuhudumia abiria milioni 140 na tani milioni 6 za mizigo, utakuwa miongoni mwa viwanja vya ndege vyenye pilika nyingi zaidi duniani.
Mamlaka hizo zimeeleza kuwa, mradi wa upanuzi wa uwanja huo umechukua miaka mitano na kugharimu yuan bilioni 53.77 (Dola za Kimarekani karibu bilioni 7.6). Pia unajumuisha kituo jumuishi cha usafiri kilichoundwa ili kuboresha muunganisho wa anga, reli na barabara.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




