

Lugha Nyingine
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lahitimisha Mjadala wa jumla
UMOJA WA MATAIFA - Mjadala wa Jumla wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umehitimishwa jana Jumatatu ambapo katika hotuba yake ya kufunga, Rais wa Baraza Kuu Annalena Baerbock amesema nchi wanachama 189 wa Umoja wa Mataifa walitoa hotuba katika Mjadala huo, wakiwemo wale wa wakuu wa nchi na serikali 124.
"Mwanzoni mwa wiki hii, tuliurejelea Umoja wa Mataifa kuwa ni nyumba ya diplomasia na mazungumzo, iliyosimama njia panda, mahali ambapo tunakusanyika kufanya mazungumzo magumu wakati wa changamoto," amesema, akiongeza kuwa kama wiki hiyo ya ngazi ya juu ni alama, nyumba hii inatimiza lengo hilo: Umoja wa Mataifa bado una umuhimu.
Amesema katika wiki nzima, kulikuwa na nyakati za nishati -- hata umeme -- ambapo nchi wanachama walihisi nia ya pamoja ya kufanya vyema zaidi, kufika mbali zaidi, kuchagua njia sahihi katika njia panda.
"Mjadala wa jumla wa wiki hii, ukiwa na maongezi mazito na maneno ya kutia moyo, umeonyesha kwamba tunao uwezo wa kutafuta nguvu kuinua uongozi wetu wa pamoja, kutafuta suluhisho la pamoja, na kuchukua njia sahihi katika njia panda," amesema.
"Hebu tuhamasishwe na urithi wa maisha yetu ya zamani, na kushirikiana kwa mustakabali mzuri wa baadaye. Bila woga. Bila kuvunjika. Tukiwa wamoja." ameongeza.
Mkutano huo wa mwaka huu umefanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa. Wiki ya Ngazi ya Juu iliwapa viongozi wa dunia fursa ya kutathmini miongo minane iliyopita na kutazama mbeleni.
Vita vinavyopamba moto katika sehemu mbalimbali duniani, ushindani wa nchi zenye nguvu, mgogoro wa janga la tabianchi, na nakisi ya maendeleo endelevu, miongoni mwa changamoto nyinginezo, vilitoa mada za kutosha kwa mjadala.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma