

Lugha Nyingine
Njia mpya ya reli ya mwendo kasi kuchochea zaidi ukuaji wa michezo ya majira ya baridi wa China (3)
![]() |
Treni inayoelekea Stesheni ya Reli ya Changbaishan ikiondoka kutoka Stesheni ya Reli ya Fushun, Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, Septemba 28, 2025. (Xinhua/Pan Yulong) |
CHANGCHUN – Njia mpya ya reli ya mwendokasi imeanza kufanya kazi jana Jumapili, ikifupisha kwa kiasi kikubwa muda wa kusafiri kutoka Beijing hadi Mlima maarufu wa Changbai katika Mkoa wa Jilin kaskazini-mashariki mwa China, ikitoa msukumo kwa soko linalokua la China la michezo ya majira ya baridi na utalii wa barafu.
Sehemu ya Shenyang-Baihe ya Reli ya Mwendokasi ya Shenyang-Jiamusi, iliyosanifiwa kupitisha treni zinazoendeshwa kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa, imeanza kutoa huduma rasmi jana Jumapili.
Njia hiyo mpya inapunguza muda wa usafiri kutoka Beijing hadi eneo la Mlima Changbai, kivutio maarufu cha utalii, chenye vituo vya hali ya juu vya michezo ya kuteleza kwenye barafu, hadi saa 4 na dakika 33 tu, ikiokoa karibu saa moja na nusu.
Ili kukidhi mahitaji ya watalii, treni zinazopita kwenye njia hiyo zimeongeza nafasi kati ya siti ili kuwezesha kuchukua vifaa vizito vya michezo ya kuteleza kwenye barafu. Mabehewa yamefungwa mfumo wa AI wa kudhibiti halijoto ili kupunguza usumbufu kutokana na mabadiliko makubwa ya halijoto ndani na nje.
Stesheni kando ya njia hiyo zinatoa kaunta za huduma jumuishi za utalii kwa ajili ya uwekaji oda zote katika kituo kimoja kwenda kutalii katika eneo la Mlima wa Changbai na kupata huduma za utalii wa watu kujiendesha wenyewe.
Kwa kuwa njia hiyo ya reli inapita katikati ya eneo la Mlima Changbai, asilimia 77 ya njia hiyo imejengwa kwa usanifu wa madaraja au mahandaki.
Mkoa wa Jilin unapatikana kati ya nyuzi 40 na 50 ya latitudo ya kaskazini, unajulikana sana kwa theluji yake ya asili, kama ya poda. Ikiwa na maeneo 68 ya michezo ya kuteleza kwenye theluji na njia 361 za kuteleza kwenye barafu zinazoenea eneo lenye ukubwa wa hekta 1,414, na urefu wa jumla wa kilomita 398, miundombinu ya Jilin ya barafu na theluji inawafaa watelezaji wa ngazi zote. Kuanzia Novemba 2024 hadi Machi 2025, Jilin ilikaribisha watalii wa ndani milioni 170, ongezeko la asilimia 35 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma