Rais wa Madagascar alaani uporaji na kutoa wito wa kujizuia (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 28, 2025
Rais wa Madagascar alaani uporaji na kutoa wito wa kujizuia
Gari na sehemu za mbele za maduka yaliyoharibiwa vikionekana kwenye picha katika eneo la manunuzi mjini Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, Septemba 26, 2025. (Picha na Sitraka Rajaonarison/Xinhua)

ANTANANARIVO - Andry Rajoelina, Rais wa Madagascar, juzi Ijumaa alilaani matukio ya vurugu yaliyotokea siku iliyotangulia ya Alhammisi, haswa katika mji mkuu, Antananarivo, huku akihimiza watu wote wa Madagascar kujizuia.

"Kutokana na matukio yaliyosababisha uporaji na uharibifu wa mali na biashara, ninalaani vitendo hivi vya uharibifu na nia ya kuongeza vurugu katika nchi yetu," rais huyo amesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii.

Maandamano yaliandaliwa siku ya Alhamisi mjini Antananarivo kupinga kukatika umeme mara kwa mara na uhaba wa maji, ambayo yalichochewa hadi kuwa uporaji katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo ya kisiwa cha Bahari ya Hindi mwishoni mwa siku hiyo.

Angelo Ravelonarivo, Gavana wa Antananarivo, alitangaza siku hiyo Alhamisi usiku marufuku ya kutoka nje kuanzia saa 1 jioni (1600 GMT) hadi 11 alfajiri (0200 GMT) katika mji mkuu na maeneo yake ya karibu, "hadi utaratibu urejeshwe."

Rajoelina, ambaye alikuwa New York, Marekani, kuhudhuria Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, amesema "mgawanyiko na chuki si suluhisho," akiongeza kuwa "makabiliano yanaleta tu uharibifu, na hakuna anayefaidika nayo isipokuwa wale wanaotafuta maslahi yao tu."

Pia amewatakia wale waliojeruhiwa kwenye matukio hayo ahueni ya haraka na kutoa wito kwa watu wote wa Madagascar endelea kujizuia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha