Mkoa wa Xinjiang, China wabadilisha majangwa kuwa sehemu adimu ya kuzalisha nishati mbadala (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 28, 2025
Mkoa wa Xinjiang, China wabadilisha majangwa kuwa sehemu adimu ya kuzalisha nishati mbadala
Picha iliyopigwa kwa droni Aprili 24, 2025 ikionyesha wafanyakazi wakikagua mradi wa njia ya kusambaza umeme wa moja kwa moja kwa volteji ya juu zaidi (UHV) unaounganisha Xinjiang na Mji wa Chongqing, kusini-magharibi mwa China katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China. (Picha na Zhang Lingjun/Xinhua)

Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, mkoa tajiri wa rasilimali za nishati za jua na upepo, umeendeleza kwa nguvu sekta ya nishati mpya katika miaka ya hivi karibuni, ikiharakisha ujenzi wa miradi mikubwa ya msingi ya kuzalisha umeme kwa nishati za upepo na jua.

"Njia ya mzunguko ya kusambaza kwa kasi umeme" wa kilovolti 750 (kV), ambayo ni njia inayopita eneo kubwa zaidi ya aina yake nchini China, imeonekana katika sehemu mbalimbali mkoani Xinjiang, ikiwa nguzo yenye ufanisi mkubwa kwa usambazaji wa nishati. Hivi leo, karibu theluthi moja ya umeme unaosambazwa mkoani Xinjiang ni nishati safi za upepo na jua. Unasambaza kilowati zaidi ya bilioni 270 za umeme wa kijani kwa mikoa mingine nchini.

Aidha, viwanda vingi zaidi vinaendeleza nishati safi katika mkoa wa Xinjiang, vikisukuma mbele maendeleo ya kijani ya mkoa huo. Aina mbalimbali za viwanda vya kutengeneza zana na vifaa vya nishati mpya mkoani Xinjiang, kama vile wafer za silicon, moduli za kuzalisha umeme kwa jua, zana na vifaa vya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo, vimekuwa vikiboreshwa siku hadi siku, na mnyororo wa viwanda umekuwa ukikamilishwa kwa kasi kubwa.

Majangwa makubwa na ardhi isiyo na tija ya Xinjiang, ambavyo hapo awali vilionekana kama vizuizi kwa uchumi, vimebadilishwa kuwa sehemu adimu ya uzalishaji wa nishati mbadala. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha