Hafla ya maonesho ya kwanza ya Filamu ya kuonesha ukatili wa Japan katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia yafanyika Harbin, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2025
Hafla ya maonesho ya kwanza ya Filamu ya kuonesha ukatili wa Japan katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia yafanyika Harbin, China
Mwanafamilia wa mhanga akitazama filamu ya “Ukatili Usio na Ukomo” huko Harbin, Mkoa wa Heilongjiang Kaskazini Mashariki mwa China Septemba 17, 2025. (Picha na Zhang Dawei/Xinhua)

HARBIN – Hafla ya maonesho ya kwanza ya filamu ya “Ukatili Usio na Ukomo” ambayo ni filamu kuhusu Kikosi cha 731 cha Jeshi la uvamizi la Japan, imefanyika Jumatano mjini Harbin, sehemu ambayo kilikuwa kituo cha kikosi hicho cha kufanya vita vya kibakteria cha Japan kilicholaumiwa vikali sana, ikionesha ukatili na uovu uliofanywa na vikosi vya Japan vya kuvamia China katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Filamu hiyo imeeleza hadithi kuhusu Wang Yongzhang, muuzaji mwenyeji wa rejareja, na watu wengine waliofungwa kwenye “jela maalumu” la Kikosi cha 731, watu hao ambao walishawishiwa na ahadi ya uwongo kuwaachilia huru baada ya kushiriki kwenye vipimo vya afya na kufanyiwa utafiti wa kuzuia maradhi, na mwishowe walikuwa wahanga wa majaribio ya kutisha ya matibabu, yakiwemo majaribio ya kujeruhiwa kwa kugandishwa kwenye barafu, kuachiwa wazi kwenye gesi ya sumu na kufanyiwa upasuaji.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Renato Lu)

Picha