Mji wa Kisayansi wa Guangming, Shenzhen, China washikilia mustakabali wa sayansi na teknolojia ukiwa umejaa usanifu wa siku za baadaye (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 18, 2025
Mji wa Kisayansi wa Guangming, Shenzhen, China washikilia mustakabali wa sayansi na teknolojia ukiwa umejaa usanifu wa siku za baadaye
Picha ikionesha usanifu wa nje wa jengo la Kituo cha Sanaa na Utamaduni cha Guangming, Shenzhen, China. (Picha/People’s Daily Online)

Mji wa Kisayansi wa Guangming katika Mji wa Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China ukiwa na usanifu mbalimbali wa miundombinu wa siku za baadaye (futuristic designs) unaelezwa kuwa wenye kiwango cha dunia.

Kuanzia uwepo wa miradi mikubwa ya kisayansi kama vile sayansi ya uigilizaji na uchambuzi wa ubongo (brain simulation and analysis), dawa za binadamu, hadi Eneo Maalumu la Sayansi ambalo ndani yake lina Jumba la Makumbusho ya Sayansi na Teknolojia la Shenzhen, Kituo cha Sanaa na Utamaduni cha Guangming, Kituo cha Michezo cha Mji wa Sayansi wa Guangming, mji huo una miundombinu mbalimbali ambayo ndani yake huunda taswira mpya yenye kujenga picha ya maisha yasiyo na mwisho.

Mathalan, Jumba la Makumbusho ya Sayansi na Teknolojia la Shenzhen katika mji huo lililofungua rasmi milango yake kwa umma mwezi Mei mwaka huu, lina muundo wa kipekee wa kisanifu wenye kufanana na anga ya juu likionyesha mambo mengi kuhusu ustaarabu wa kidijitali, AI, roboti za michezo mbalimbali ya kuchemsha ubongo na akili na teknolojia ya mawasiliano.

Ndani yake, watembeleaji wanaweza kuona vitu changamani na wanavyoweza kujumuika navyo kuhusu teknolojia mpya za kisasa kama vile AI na uchunguzi wa anga ya juu, ambavyo vimepangiliwa kwa namna ambayo inawapa elimu na kujenga hamasa.

Aprili 2020, Serikali ya Mji wa Shenzhen ilitoa Mawazo Kadhaa juu ya Kuunga Mkono Ujenzi wa Mji wa Sayansi wa Guangming kuwa Mji wa Sayansi wa Kiwango cha Juu Duniani. Kwa kutilia maanani maono ya kimataifa, viwango vya kimataifa, unaalum wa China na nafasi ya maendeleo ya teknolojia ya hali ya juu, Serikali ilitangaza kuujenga mji huo kuwa eneo la msingi la kubeba kazi za Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao.

Hadi kufikia mwaka 2022, mji huo tayari ulikuwa umechukua taswira na kuwa kituo cha kitaifa cha sayansi cha China. Itakapofika mwaka 2035, mji huo unalenga kuwa mji wa sayansi wa kiwango cha juu duniani ukiwa na uwezo wa ushindani mkubwa.

Taarifa iliyotolewa na Serikali ya Mji wa Shenzhen inaonesha kuwa mwaka huu mji huo wa kisayansi umefikia hatua ya aina yake kwa kupata nafasi ya 7 kwenye orodha ya Miji 100 Bora nchini China kwa maendeleo ya Sayansi na Teknolojia. Ulikuwa katika nafasi ya 15 mwaka 2023 na 24 mwaka 2022.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha