

Lugha Nyingine
Ghana yaandaa mkutano wa kilele kwa wito wa kufikia na kupanga upya mfumo wa afya duniani
![]() |
Rais John Dramani Mahama wa Ghana (Nyuma kulia) akitoa hotuba kwenye Mkutano wa Afya wa Afrika mjini Accra, Ghana, Agosti 5, 2025. (Xinhua/Seth) |
ACCRA, Agosti 5 (Xinhua) -- Mkutano wa kilele wa Mamlaka ya Afya Afrika ulifunguliwa Jumanne huko Accra, Ghana, na kutoa wito wa kufikiria na kupanga upya usimamizi wa afya duniani katika wakati wa kukabiliwa na mabadiliko ya haraka ya siasa ya kijiografia na muundo wa uchumi. Mkutano huo ulioitishwa na Rais John Dramani Mahama wa Ghana, unalenga kuandaa zama mpya za mamlaka ya afya zinazokita mizizi kwenye msingi wa nchi kujiamulia, kufanya uwekezaji na kuwa na uwezo wa uongozi.
Rais Mahama ametoa wito kwa juhudi za kubadilishwa usanifu ambao umeondoa sauti ya Afrika, mahitaji na ubunifu wakati wa ufunguzi wa mkutano. Rais wa Ghana amesema Afrika inahitaji kuunda mfumo wa afya ambao sio tu unaweza kukabiliana na majanga ya afya, bali pia unaweza kuwa wa uwezo wa ufufukaji baada ya majanga , wenye kuhimiza usawa, na kuimarisha utu wa watu wake, na ametoa wito wa kutumia mbinu mpya ya ufadhili wa afya katika bara la Afrika.
Rais Mahama amesema,“Ninatoa mwito wazi kwa nchi zote zilizowakilishwa hapa kuungana nasi katika kujenga mfumo ikolojia wa uwekezaji wa afya barani Afrika ambao unaendeshwa kwa usawa na kwenye mamlaka ya nchi ”.
Watu mashuhuri akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Adhanom Ghebreyesus na maofisa wakuu kutoka nchi nyingine za Afrika, pia walihudhuria mkutano huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma