

Lugha Nyingine
Uganda na Misri zajadili matumizi ya mto Nile na ushirikiano wa kikanda
KAMPALA, Agosti 5 (Xinhua) – Taarifa iliyotolewa jumanne na Ikulu ya Uganda inasema, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Bw. Badr Abdelatty aliyefanya ziara nchini Uganda wamefanya mazungumzo kuhusu matumizi ya maji ya Mto Nile na ushirikiano wa kikanda.
Kwenye mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye Ikulu ya Uganda, viongozi hao wawili walijadili wasiwasi wa Misri kuhusu usalama wa maji ya mto Nile. Rais Museveni alisema kupitia akaunti yake ya X, walijadili masuala kadhaa kuhusu Mto Nile na jinsi nchi wadau zinavyoweza kushirikiana ili kuuhifadhi, na kuutumia vyema mto huo.
Rais Museveni amesema tatizo linaloukabili Mto Nile ni ukosefu wa umeme katika nchi za tropiki. Jamii kama Fellahin itatumia miti kupika, na hivyo kuharibu majani, ambayo mwishowe yanaathiri mifumo ya mvua na kuumiza maji ya Mto Nile, na hatari ya pili ni kilimo cha kizamani.
Rais Museveni alitoa wito kwa nchi katika eneo la mtiririko wa Mto Nile kushiriki katika mjadala wa namna ya kutumia mto huo kwa njia endelevu bila kuhatarisha mustakabali wake.
Bw. Abdelatty alionyesha uwezekano wa kuwepo kwa miradi ya pamoja, inayoungwa mkono na utaratibu wa ufadhili ulioanzishwa hivi karibuni na Misri, ili kuhimiza maendeleo katika nchi za kusini mwa eneo la mto Nile. Pia ameipongeza Uganda kwa mchango wake katika kazi za kulinda amani nchini Somalia na katika nchi nyingine za Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma