ChinaVumbuzi | Roketi ya China ya Long March-12 yarusha satelaiti mpya za Internet

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 05, 2025
ChinaVumbuzi | Roketi ya China ya Long March-12 yarusha satelaiti mpya za Internet
Roketi ya Long March -12 iliyobeba kundi la setilaiti za internet ikirushwa kutoka kwenye kituo cha kurushia vyombo vya anga ya juu kibiashara Mkoani Hainan, China, Agosti 4, 2025. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

WENCHANG -- China ilirusha roketi ya Long March-12 Jumatatu, na kupeleka angani kundi la satelaiti za mtandao wa internet. Roketi hiyo ilirushwa saa 6:21 jioni kutoka kwenye kituo cha kurushia vyombo vya anga ya juu kilichoko kwenye kisiwa cha Hainan, China.

Roketi hiyo ilifanikiwa kufikisha kundi la saba la satelaiti za mtandao wa internet kwenye obiti ya chini ilivyopangwa kabla. Kwa mujibu wa kituo cha kurushia vyombo hivyo, huu ni urushaji wa 587 kwa kutumia roketi za Long March.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha