

Lugha Nyingine
Mawimbi ya joto kali yaikumba Misri, yakisababisha tahadhari nyingi (5)
![]() |
Watu wakipoza joto la mwili kwenye ufukwe wa Bahari ya Mediterania wakati wa wimbi la joto mjini Alexandria, Misri, Julai 16, 2025. (Xinhua/Ahmed Gomaa) |
CAIRO - Misri inakabiliwa na wimbi la joto kali lisilo la kawaida, huku halijoto ya juu na unyevunyevu vikihatarisha afya ya umma na kuathiri sekta muhimu kama vile kilimo na viwanda ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa ya nchi hiyo imesema kwamba halijoto jana Jumatano katika pwani za kaskazini ilikuwa kati ya nyuzi joto 31 hadi 32, katika Cairo Kuu kutoka nyuzi 37 hadi 38, na katika eneo la kusini kutoka nyuzi 40 hadi 44.
Joto hilo kali linakadiriwa kuendelea katika siku zijazo, huku halijoto ya mchana na usiku ikitabiriwa kuongezeka kwa hadi nyuzi joto 3 juu ya wastani wa msimu huu, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uchambuzi na Utabiri wa Hali ya Hewa katika Mamlaka hiyo, Mahmoud Shahin.
Ibrahim Darwish, profesa wa Kilimo katika Chuo Kikuu cha Menoufia, Misri amesema kuwa kupanda kwa joto kunaleta changamoto kubwa kwa usalama wa chakula na maji katika nchi za kilimo.
Ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa joto la juu husababisha kupungua kwa uzalishaji wa kilimo kutokana na athari zao mbaya kwenye photosynthesis, kupumua, na biosynthesis ndani ya mimea. Darwish amesema kuwa wimbi la joto huenda litabadilisha nyakati za kupanda na kukomaa, kwani halijoto ya juu huharakisha mzunguko wa maisha ya mmea, ikisababisha kukomaa kabla ya muda na kusikokamilika, ambayo kwa upande wake huzuia kuumbika vya kutosha kwa vitu kavu, hasa kwenye nafaka.
Mhandisi Ahmed Abdel-Rashid, meneja wa kiwanda cha viyoyozi katika Haier Egypt Environmental Complex, amesema joto la juu litasababisha kupungua kwa ufanisi wa kazi na kuongeza hatari ya ajali mahali pa kazi.
Abdel-Rashid amesema kuwa wimbi la joto pia litasababisha matumizi ya juu ya umeme kutokana na kuongezeka kwa utegemezi wa mifumo ya kupoza, na kuongeza hatari ya kuharibika kwa mashine zenye udhaifu kwa joto, na uwezekano wa kusababisha ucheleweshaji wa uzalishaji au kufungwa.
Magdy Badran, mwanachama wa Jumuiya ya Aleji na Kinga ya Misri, amesema miongoni mwa athari mbaya zaidi za kiafya ambazo wananchi wanaweza kupata wakati wa wimbi la joto la sasa ni shinikizo la joto na kiharusi cha joto.
"Hizi ni miongoni mwa hatari za kiafya za kawaida katika hali ya hewa ya joto, zinazotokana na mwili kupoteza kiasi kikubwa cha maji na chumvi kutokana na kutokwa jasho kupindukia, ikisababisha kizunguzungu, maumivu ya kichwa, kichefuchefu, na uchovu wa mwilini. Kama haitashughulikiwa haraka, hali inaweza kuongezeka na kusababisha kiharusi cha joto," ameliambia Xinhua.
Wilaya ya Xuan’en yahimiza utalii wa usiku kando ya Mto Gongshui Katikati mwa China
Eneo la mtaa mkongwe lawa na ustawi kwa uvumbuzi wa kitamaduni na utalii mkoani Jiangxi, China
Mji wa Tianjin, China waharakisha ufungamanishaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi halisi
Ardhioevu yalinda spishi za ndege kutoka kwenye uwanda hadi mijini
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma