

Lugha Nyingine
Mkoa wa Guizhou, China wajitahidi kubadilisha nguvu bora ya kiikolojia kuwa nguvu bora ya maendeleo
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2025
Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Guizhou, Kusini-magharibi mwa China umepata maendeleo makubwa katika ujenzi wa ikolojia, ukijitahidi kubadilisha nguvu bora ya kiikolojia kuwa nguvu bora ya maendeleo.
Mkoa wa Guizhou ukiendeleza nishati ya kijani kama vile nishati ya upepo na jua, pia umetumia vya kutosha ardhi iliyo chini ya paneli za kuzalisha umeme kwa jua kulima mimea ya mazao, na wakati huo huo unahimiza wakulima kupanda mimea ya mazao ya kilimo kwa kutumia miinuko mbalimbali ya ardhi na tabianchi mbalimbali, ili kuongeza mapato ya wakulima.
Hivi sasa, ukubwa wa eneo la misitu la mkoa huo wa Guizhou unafikia asilimia 63.3, na uchumi wake wa kijani unachangia asilimia 48 ya muundo wa jumla wa uchumi wa mkoa huo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma