

Lugha Nyingine
Vikosi vya manowari za China vyarejea baada ya kumaliza mafunzo kwenye bahari ya mbali
BEIJING – Vikosi vya manowari mbili za China, Liaoning na Shandong, vimemaliza mafunzo yao ya kivita katika bahari ya mbali na kurejea salama katika bandari zao za nyumbani, Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) kimesema katika taarifa yake iliyotolewa jana Jumatatu.
Taarifa hiyo imesema kuwa, mafunzo hayo yaliendeshwa kwa namna iliyoratibiwa na kupangiliwa vema kwani manowari hizo mbili zilisonga mbele kuingia Bahari ya Pasifiki ya Magharibi, kushirikiana na vikosi husika vya kijeshi, na kukamilisha mazoezi mbalimbali chini ya hali ya mapigano, kama yale yanayohusiana na upelelezi na tahadhari ya mapema, shambulizi la baharini, ulinzi wa anga, na urukaji kiufundi wa mchana na usiku wa ndege zilizobebwa kwenye manowari hizo.
"Mafunzo yamepata mafanikio mbalimbali ya utafiti kwa masomo husika ya kijeshi na kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kimfumo wa kivita wa manowari hizo za China, kufuatia mazoezi ya hapo awali ya vyombo hivyo viwili yaliyofanywa kwa pamoja na vikosi hivyo viwili vya jeshi la majini mwaka jana," imesema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakati wa mafunzo hayo, baadhi ya meli na ndege za kivita za kigeni mara kadhaa zilifanya upelelezi, ufuatiliaji na kurekodi mambo kwa ukaribu.
"Vikosi vya manowari vya China vilidumisha umakini na mwitikio wa hali ya juu kwa mazingira ya vita, kupanga safari kadhaa za ndege zilizokuwa kwenye manowari, na kushughulikia hali hiyo kwa weledi na umakini," imeeleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Kikosi cha Majini cha PLA, kama utaratibu wa kawaida wa mpango wake wa mwaka, mafunzo hayo yamejaribu kwa ufanisi matokeo ya mafunzo ya pamoja ya vikosi husika na kuongeza uwezo wao wa kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya nchi.
Kituo cha mafunzo cha Bajiquan mkoani Hebei, China chakaribisha wanafunzi kutoka Russia
Picha: Mandhari ya mbuga katika majira ya joto mkoani Gansu, China
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma