

Lugha Nyingine
Bandari ya mpakani magharibi zaidi mwa China yaanza kufanya kazi saa 24 kila siku ili kuhimiza biashara ya Asia ya Kati
URUMQI - Bandari ya Irkeshtam katika Wilaya ya Wuqia ya Eneo linalojiendesha la Kirgiz la Mji wa Kizilsu, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China imeanza kufanya majaribio ya kutoa kibali cha usafirishaji wa mizigo kwa saa 24, ikiifanya kuwa bandari ya pili ya nchi kavu katika mkoa huo na ya kwanza kusini mwa Xinjiang kupitisha mfumo wa aina hiyo. Hatua hiyo inalenga kuimarisha usafirishaji wa bidhaa za biashara kati ya China na Asia ya Kati, kituo cha ukaguzi wa uhamiaji cha eneo hilo kimeeleza.
Ikiwa ni bandari ya nchi kavu ya magharibi zaidi mwa China, Irkeshtam inatumika kama mlango muhimu wa kuelekea Kyrgyzstan na kituo muhimu cha Asia ya Kati na Magharibi, ambapo shughuli za kuvuka mpaka zinaongezwa siku hadi siku, na mahitaji makubwa ya usafirishaji bidhaa pia yanaongezwa kwa nguvu.
Ili kuunga mkono shughuli za kila saa, kituo cha ukaguzi wa uhamiaji cha Irkeshtam kimeboresha upangaji wa wafanyakazi, kwa kupitia zamu za mzunguko na kutekeleza "ukaguzi wakati wa kuwasili" kwa magari ya mizigo, hali ambayo imeleta uwiano kati ya usalama na ufanisi.
Jiang Zhidong, meneja mkuu wa Kampuni ya Biashara ya Kimataifa ya Xinjiang Jiujiuxi, ambayo makao yake makuu yako mjini Kashgar, amesema kuwa mfumo huo utaongeza ufanisi wa usafirishaji wa shehena, kupunguza gharama za uchukuzi, kuchochea zaidi uhai wa shughuli za bandari na kutumia ipasavyo nguvu na uwezo wa biashara na nje.
Takwimu zinaonyesha kuwa usafirishaji wa mizigo umeongezeka sana mwaka huu katika bandari hiyo ya Irkeshtam, huku kituo hicho kikishughulikia usafiri wa mara zaidi ya 105,800 wa magari 98,500 hadi kufikia Jumapili iliyopita, ongezeko lilifikia asilimia 80 na asilimia 79 zaidi kuliko mwaka uliopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma