Hali ya maendeleo ya Mji wa Nagqu, Xizang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 09, 2025
Hali ya maendeleo ya Mji wa Nagqu, Xizang, China
Picha iliyopigwa tarehe 12 Julai 2022 ikionyesha mandhari ya mapema asubuhi ya mashambani katika Tarafa ya Doima ya Wilaya ya Shuanghu ya Mji wa Nagqu, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua/Jigme Dorje)

Katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China, unaojulikana kama "paa la dunia," kuna sehemu inayoitwa Nagqu, kimvuto ikiitwa "paa la paa la dunia." Ukiwa kwenye mwinuko wa juu zaidi kuliko mji wowote wa China, mji huo wa ngazi ya wilaya mkoani Xizang, wastani wa mwinuko wa sehemu zake zote umezidi mita 4,500 kutoka usawa wa bahari.

Mji huo wa Nagqu unajulikana kwa mazingira yake ya kipekee, hali ya hewa ya nusu kame na udongo wa mchanga, na hapo zamani ulikuwa mji pekee wa ngazi ya wilaya nchini China usio na miti kwa ajili ya kujenga mazingira ya kijani mjini. Baada ya miaka ya juhudi nyingi, kuonekana kwa miti si anasa tena isiyoweza kufikiwa mjini Nagqu. Aina mbalimbali za miti imeishi hapa na inakua kando za barabara. Ujengaji mazingira ya kijani mjini pamoja na mambo mengine mengi ya maendeleo ya mji huo unaboreshwa kwa kasi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha