

Lugha Nyingine
Utalii maalum wa kitamaduni na mandhari nzuri ya Mto Manjano vyavutia watalii Xin'an, China (3)
![]() |
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya kigeni wakijaribu kupiga ala ya muziki ya jadi ya Guzheng. (Picha iliyotolewa na Kituo Jumuishi cha Vyombo vya Habari cha Wilaya ya Xin'an) |
Tarehe 24 Aprili, ziara ya Vyombo vya Habari vya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" katika Mkoa wa Henan, China yenye kauli mbiu ya "Harufu Nzuri ya Maua ya Peony kwenye Njia Mpya ya Hariri", ambayo inaandaliwa na People's Daily Online, iliingia kwenye Eneo la Kupiga Kambi la Mlima Yingzui katika Wilaya ya Xin'an ya Mji wa Luoyang wa mkoa huo.
Eneo la Kupiga Kambi la Mlima Yingzui likiwa eneo kuu la shughuli hiyo, limeshuhudia mabadiliko ya kupendeza katika utalii wa kitamaduni wa Xin'an. Zamani lilikuwa ni mteremko uliotelekezwa, lakini sasa limesifiwa mtandaoni kuwa "mahali mashuhuri pa kupiga picha kwa watalii" panapopatikana kando za Mto Manjano.
Kuna sehemu za kutazama sinema kwa kukaa ndani ya gari, vibanda vya msituni, kupiga kambi na kula nyama choma, na shughuli ya burudani ya kuvulia samaki kwa ndoano. Watalii wanaweza pia kupanda maputo ya kupaa angani na kushiriki kwenye shughuli zingine ili kutazama Sura nzuri ya Mto Manjano kutoka mawinguni.
Msimamizi wa Idara ya Utamaduni, Redio, Filamu na Utalii ya Wilaya ya Xin'an amesema, "Katika hatua inayofuata, tutaendelea kuboresha miundombinu kwa ajili ya shughuli za utalii na kualika kwa dhati marafiki wa ndani na nje ya China kuja Xin'an na kufurahia mvuto wa Mto Manjano!"
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma