Banda la China lavutia watu wengi kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Zimbabwe (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2025
Banda la China lavutia watu wengi kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Zimbabwe
Mwanamke wa Zimbabwe akifahamishwa kuhusu dawa za jadi za China kwenye banda la China katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Zimbabwe mjini Bulawayo, Zimbabwe, Aprili 24, 2025. (Xinhua/Xu Zheng)

BULAWAYO, Zimbabwe - Banda la China limevutia watembeleaji wengi kwenye Maonyesho ya 65 ya Kimataifa ya Biashara ya Zimbabwe (ZITF) yanayoendelea mjini Bulawayo, jiji la pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe ambapo yakiwa ni maonyesho maarufu ya mwaka ya Zimbabwe, maonyesho hayo ya mwaka huu yaliyoanza Jumatatu wiki na yamepangwa kuendelea hadi kesho Jumamosi -- yamevutia waonyeshaji bidhaa zaidi ya 600 kutoka duniani kote.

Maonyesho hayo ya mwaka huu yamegongana na maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Zimbabwe, mashirika na kampuni mbalimbali za China zinashiriki katika maonyesho hayo, zikiwasilisha vitu na bidhaa mbalimbali na maonyesho ya utamaduni kwenye Banda la Maonyesho la China.

"Nilikuwa nikiona maandishi ya kichina kwenye filamu za sanaa za Kung Fu za China nilipokuwa mtoto, na muda wote imekuwa ikinivutia. Imekuwa hali ya kusisimua sana kupata fursa ya kujaribu hapa. Ni njia maalum ya kuunganisha uhusiano wa kitamaduni kati ya China na Zimbabwe," Leon Bare, mfanyabiashara mwenyeji na muonyeshaji bidhaa ambaye ametembelea Banda la China, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua jana Alhamisi.

Mtembeleaji mwingine, Gamuchirai Chiduwa, amejaribu kuandika maandishi ya Kichina kwa mara ya kwanza, na anaona uzoefu wake huo ni wa kufurahisha na unafungua macho yake.

Kama sehemu ya mawasiliano ya kitamaduni, watembeleaji pia wamehudumiwa kwa aina mbalimbali za chai za Kichina. Mkazi mwenyeji Tawanda Maruza, ambaye aliingia ndani ya banda hilo pamoja na familia yake, amesema, "Watoto wameonja chai ya Kichina na wakaipenda. Natumai hii itaibua shauku yao ya kujifunza zaidi kuhusu utamaduni wa China."

Wataalamu wa tiba kutoka kundi la 22 la timu ya madaktari ya China nchini Zimbabwe pia wanaonyesha mbinu za dawa za jadi za China, zikiwemo tiba ya acupuncture na kikombe, ikivutia shauku ya watu wengi.

"Sijawahi kusikia kuhusu tiba ya acupuncture hapo awali, hivyo nashukuru kwa fursa hii ya kujionea utamaduni wa China kwa pamoja. Kutembelea kwangu hapa kumenidhihirishia mambo mengi ambayo sikuyajua," amesema mtembeleaji Eric Mvurumutiya.

Kwa mujibu wa Ubalozi wa China nchini Zimbabwe, hafla maalum ya Siku ya China itakuwa ikifanyika leo Ijumaa, ili kuwapa watembeleaji fursa ya kujihusisha na shughuli nyingi zaidi za kitamaduni na kuzidisha ufahamu wao juu ya China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha