

Lugha Nyingine
Maisha ya Tumbili adimu wa dhahabu kwenye Eneo la Urithi wa Dunia wa Mazingira ya Asili la China (4)
Tumbili adimu wa pua fupi, au tumbili wa dhahabu wa Guizhou, kipekee wanaopatikana ndani ya eneo kubwa la Mlima Fanjing, Eneo la Urithi wa Dunia wa Mazingira ya Asili la UNESCO, yupo chini ya ulinzi wa ngazi ya juu zaidi nchini China na ameorodheshwa kama spishi zilizo “hatarini sana” na Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira ya Asili.
Miongoni mwa spishi tatu za tumbili wa pua fupi ambazo zinapatikana kipekee nchini China, tumbili huyo wa pua fupi wa Guizhou ndiye mwenye idadi ndogo zaidi, maskani madogo zaidi na taarifa chache zaidi za kiikolojia.
Takwimu kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Mazingira ya China zinaonesha kuwa, kwa sasa kuna tumbili tisa wa pua fupi wa Guizhou wanaolelewa kwenye Kituo hicho cha Utafiti wa Tumbili wa Pua Fupi wa Guizhou cha Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Mlima Fanjing.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma