Mkoa wa Shanxi, China wafanya juhudi kubwa kulinda na kutafiti Mapango ya Yungang (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2025
Mkoa wa Shanxi, China wafanya juhudi kubwa kulinda na kutafiti Mapango ya Yungang
Watalii wakitembelea Mapango ya Yungang mjini Datong, Mkoani Shanxi, kaskazini mwa China, Aprili 15, 2025.(Xinhua/Zhan Yan)

Mapango ya Yungang katika Mkoa wa Shanxi, kaskazini mwa China yalijengwa wakati wa Enzi ya Wei Kaskazini (mwaka 386-534) ya China. Huchukuliwa kuwa kilele cha sanaa ya Kibuddha ya China na yanawakilisha kiwango cha juu zaidi cha usanii wa sanamu za kuchongwa duniani wakati wa karne ya 5.

Katika miaka ya hivi karibuni, mkoa huo wa Shanxi umekuwa ukifanya juhudi kubwa kulinda na kutafiti mapango hayo. Mwaka 2021, taasisi ya utafiti ya Mapango ya Yungang ilianzishwa kwa ajili ya ulinzi, utafiti na usimamizi wa mapango hayo.

Tangu mwaka 2003, Eneo hilo la Urithi wa Dunia wa UNESCO limeanza kazi ya kuweka rekodi ya kidijitali mapango yake makubwa 45 na sanamu zaidi ya 59,000 za mawe ambazo zinatishiwa na hali ya hewa. Teknolojia ya kisasa imetumika kurekodi maelezo ya kazi hizo za sanaa za Kibuddha, kwa ajili ya kazi yao ya kujenga upya kwa kutumia teknolojia ya kidijitali ya 3D.

Kwa sasa, eneo hilo la kivutio cha watalii la Mapango Yungang limeboresha miundombinu ya utalii na linatoa shughuli mbalimbali za elimu, likiwa lilipokea watalii milioni 4.44 mwaka 2024. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha